ODAMA KUZINDUA FILAMU KITOFAUTI

ODAMA KUZINDUA FILAMU KITOFAUTI

451
0
KUSHIRIKI

NA JEREMIA ERNEST (DSJ)

STAA wa filamu za kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’, leo anatarajia kuzindua filamu yake inayoitwa Mr Kiongozi kitofauti, kupitia mfumo mpya wa Kampuni ya Maxicom Africa (Maxi Malipo), utakaowezesha kusambaza kazi kwa urahisi.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Odama alisema mfumo huo una lengo la kuinua kazi za sanaa kwa kurahisisha usambazaji kutoka kiwandani mpaka kuwafikia walaji, ambao ndio mashabiki.

“Huu ni mzuri, kwani utarahisisha kusambaza kazi zetu kuwafikia mashabiki ambapo kesho (leo) nitazindua filamu yangu ya Mr Kiongozi na nitawafahamisha namna inavyoweza kupatikana,” alisema Odama.

Mfumo huo unatarajiwa kuzinduliwa leo katika ukumbi wa Kisenga LAPF, kuanzia saa 4 asubuhi, huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU