SNURA AAHIDI KURUDI TENA KIBITI

SNURA AAHIDI KURUDI TENA KIBITI

412
0
KUSHIRIKI

NA KYALAA SEHEYE

MAPOKEZI makubwa aliyoyapata msanii wa Bongo Fleva, Snura katika Wilaya ya Kibiti, mkoani Pwani, katika kampeni ya kuelimisha madhara ya unywaji dawa kiholela, staa huyo ameahidi kurudi tena wilayani humo.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Snura alisema mapokezi hayo makubwa yalimfanya atoe machozi ya furaha na kuahidi kurudi tena Kibiti na kudondosha shoo ya bure.

“Kwa kweli mapokezi niliyoyapata Kibiti yamenifanya nilie na nitoe ahadi ya kurudi tena kuwapa shoo ya bure kwa kuwa walionyesha hamu kubwa sana kutokana na kukosa burudani muda mrefu,” alisema Snura.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU