MIUJIZA USAJILI YANGA

MIUJIZA USAJILI YANGA

3445
0
KUSHIRIKI

HUSSEIN OMAR NA SAADA SALIM


KUNA msemo wa Kiswahili usemao ‘ukweli mchungu’. Hivyo ndivyo ilivyo ndani ya Yanga, kwani kwa hali ilivyo kuhusiana na suala zima la usajili, ni miujiza pekee inayoweza kuifanya klabu hiyo kufurukuta katika dirisha dogo la usajili, zikiwa zimesalia saa chache kabla ya kufungwa saa sita usiku leo.

Pamoja na mbwembwe na tambo kutoka kwa baadhi ya viongozi na ‘matajiri’ wa klabu hiyo juu ya wachezaji waliokuwa wametangaza kuwanasa kutoka ndani na nje ya Tanzania, lakini hadi sasa kiza kinene kimetawala juu ya mchakato huo.

Kati ya wachezaji ambao walitajwa kuwa mbioni kutua Yanga kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, wapo mshambuliaji wa Prisons, Mohammed Rashid, kiungo wa Mtibwa Sugar, Mohammed Issa ‘Mo Banka’, mshambuliaji wa Njombe Mji, Ditram Nchimbi, mshambuliaji wa Mbao FC, Habib Haji na wengineo.

Lakini pia, wapo wale wa kigeni, beki wa Mbao FC, Yusuph Ndikumana, Mercerin Koupko kutoka Benin, Walter Bwalya (Zambia) na Ovella Ochieng (Kenya).

Lakini majina yote hayo yanaelekea kuyeyuka Jangwani, kutokana na ukata unaowakabili mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini pia wakiwa ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

Ukweli ni kwamba, pamoja na mikakati yote iliyokuwa imetangazwa na viongozi wa Yanga juu ya usajili wao wa dirisha dogo, hadi jana hali ilikuwa tete kiasi kwamba uwezekano wa kusajili mchezaji yeyote wa kiwango cha juu ulikuwa ni finyu mno, kutokana na ukosefu wa fedha.

Hivyo, wachezaji kama Mo Rashid, Mo Banka na wengineo ambao tayari walishaweka wazi shauku yao ya kuichezea Yanga ligi itakapoendelea baada ya usajili wa dirisha dogo, itahitajika miujiza kwa wakali hao kuungana na akina Ibrahim Ajib Jangwani.

Habari za uhakika ambazo Bingwa imezinasa kutoka kwa mmoja wa vigogo wa Yanga aliyepo katika Kamati ya Mashindano, zinasema mpaka jana mchana, kulikuwa na vikao vizito kati ya Kamati ya Utendaji na Kamati ya Usajili kujadili ni namna gani wanavyoweza kufanya miujiza kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa.

“Hali ni mbaya sana, watu wameikimbia timu, waliojifanya wana mipango wakati Mwenyekiti yupo madarakani, sasa hivi hawaonekani, nampongeza Katibu Charles Boniface Mkwasa kwa juhudi zake anazozifanya ndani ya klabu,” alisema…….

Kwa habari zaidi pata nakala yako ya BINGWA

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU