FAINALI KLABU BINGWA YA DUNIA… MADRID KUENDELEZA UBABE WAO?

FAINALI KLABU BINGWA YA DUNIA… MADRID KUENDELEZA UBABE WAO?

550
0
KUSHIRIKI

ABU DHABI, UAE


TIMU ya Gremio ya Brazil inaisubiri kwa hamu Real Madrid kwenye fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia itakayofanyika kesho mjini Abu Dhabi nchini UAE.

Baada ya Real Madrid kuichapa Al Jazira mabao 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa juzi Jumatano, wanaelekea kwenye fainali nyingine huku wakiwa hawajawahi kupoteza mchezo kwenye hatua hiyo tangu mwaka 2000.

Novemba 29 mwaka 2000, ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa wafalme hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kupoteza dhidi ya Boca Juniors kwa mabao 2-1 mjini Tokyo, lakini hawajafungwa kwenye fainali 11 walizocheza ugenini tangu kipindi hicho.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wamezichapa Bayer Leverkusen, Juventus na Atletico Madrid mara mbili kila moja.

Kwenye michuano ya UEFA Super Cup, Feyenoord, Manchester United na Sevilla nao wamechapwa mara mbili, wakati Olimpia, San Lorenzo na Kashima walishindwa kuisimamisha Real Madrid na kutawazwa klabu bingwa wa dunia.

Wakati wamepoteza Kombe la Mfalme na Kombe la Hispania karne hii, Real Madrid hawana utani linapokuja suala la mataji ya kimataifa.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU