JIKE SHUPA ARUDI KUUZA CHAKULA

JIKE SHUPA ARUDI KUUZA CHAKULA

560
0
KUSHIRIKI

NA JEREMIA ERNEST (DSJ)


MREMBO aliyejizolea umaarufu baada ya kuonekana kwenye video ya msanii, Nuh Mziwanda, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’, ameamua kurudia kazi yake ya zamani ya kuuza chakula na kukisambaza kwenye ofisi mbalimbali za jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Jike Shupa, alisema ameamua kufanya uamuzi huo ili kujiongezea kipato na kuondokana na utegemezi wa kutegemea sanaa peke yake.

“Hii biashara ndiyo niliyokuwa nafanya zamani, ila nilipumzika tu kwa sasa nimeamua kurudi na nimeiboresha kwa sababu zamani nilikuwa nauza mgahawa tu ila sasa hivi napika katika sherehe, misiba na kuchukua oda katika ofisi mbalimbali,” alisema Jike Shupa.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU