WACHEZAJI UJERUMANI WAAHIDIWA BINGO

WACHEZAJI UJERUMANI WAAHIDIWA BINGO

225
0
KUSHIRIKI

MUNICH, Ujerumani


WACHEZAJI wa timu ya Taifa ya Ujerumani wameahidiwa kila mmoja kulamba kitita cha Euro 350,000 kila mmoja endapo watafanikiwa kutetea ubingwa wao wa Kombe la Dunia katika fainali zitakazofanyika mwakani nchini Urusi.

Kocha wa timu hiyo, Joachim Low, ndiye aliyeiongoza Die Mannschaft kutwaa ubingwa wa nne wa fainali hizo zilizofanyika mwaka 2014 nchini Brazil, baada ya bao lililofungwa katika dakika za muda wa nyongeza na staa Mario Gotze kuiwezesha kuilaza Argentina kwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali.

Kikiwa kimeboreshwa kwa kuongezwa nguvu ya kizazi kipya, Ujerumani na kocha wao, Low, kama watafanikiwa itakuwa ni timu ya kwanza kutetea taji hilo tangu Brazil ilipofanya hivyo mwaka 1962.

Endapo itashika nafasi ya pili, kila mchezaji atazawadiwa Euro 200,000, nafasi ya tatu kila mmoja atapewa Euro 150,000.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU