‘HATUACHANI’ YA RAY C YAMFIKIA DON JAZZY

‘HATUACHANI’ YA RAY C YAMFIKIA DON JAZZY

860
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya kuusifia wimbo wa Chura ulioimbwa na Snura, bosi wa lebo ya Mavin Records ya huko Nigeria, Don Jazzy, ameimwagia sifa ngoma mpya ya Rehema Chalamila ‘Ray C’, inayoitwa Hatuachani.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Ray C, alisema Don Jazzy alimtumia ujumbe wa kumpongeza katika ukurasa wake wa Instagram (DM), jambo ambalo limempa nguvu ya kuendelea kutoa kazi nzuri zaidi.

“Don Jazzy ni mtu mkubwa sana kwenye muziki Afrika, ujumbe wake umenipa nguvu ya kuendelea kutoa nyimbo nzuri zaidi, nimeanza na audio, video itakuja hivi karibuni,” alisema Ray C ambaye anajiandaa kufanya ziara nchini Kenya kuanzia Desemba 23, mwaka huu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU