AMBER LULU: NIACHIENI PREZZO WANGU

AMBER LULU: NIACHIENI PREZZO WANGU

659
0
KUSHIRIKI
NA JEREMIA ERNEST

VIDEO vixen na msanii wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’, amewataka mashabiki wasimhusishe mpenzi wake mpya, Prezzo, kutoka Kenya kwa kumfananisha na rapa mdogo, Young Dee.

Amber Lulu amesema anachukizwa na baadhi ya watu wanaomfananisha mpenzi wake huyo na Young Dee kwani wawili hao ni watu tofauti na hawafanani chochote.

“Wasimfananishe mume wangu na watu wengine, wanakuwa wanamkosea adabu Prezzo, kwani ni watu wawili tofauti na hawaendani hata kidogo, waache hayo mambo,” alisema Amber Lulu ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya, Kumoyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU