KANE, SANCHEZ WAKIZEMBEA TU IMEKULA KWAO

KANE, SANCHEZ WAKIZEMBEA TU IMEKULA KWAO

461
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


 

HARRY Kane na Alexis Sanchez ni baadhi ya mastaa wa Ligi Kuu England ambao wakizembea na kufanya makosa yatakayowagharimu kadi moja tu wikiendi hii, basi watajikuta wakikosa mechi zijazo.

Nyota wengine ambao jambo hilo litawagharimu kwa kiasi kikubwa ni Ashley Young, Ander Herrera na Marcos Rojo wa Manchester United, beki ambaye amecheza mechi nne tu tangu alivyopona.

Vinara wa Ligi Kuu, Manchester City, nao wana wachezaji walio hatarini kukosa mechi za wikiendi ijayo, Vincent Kompany, Fernandinho na Leroy Sane.

Kwingineko, Arsenal wana Sanchez na Granit Xhaka, Spurs wana Kane na Jan Vertonghen, wakati Liverpool wana Dejan Lovren tu.

Kanuni za Chama cha Soka England, FA, zinasema kwamba, mara baada ya mchezaji kuoneshwa kadi tano za njano anakumbana na adhabu ya kukosa mchezo mmoja wa ligi.

Adhabu hiyo hutolewa kwa wachezaji waliooneshwa kadi tano, 10 na 15 za njano ndani ya msimu.

Lakini, kanuni hiyo haitamhusu mchezaji aliyeoneshwa kadi ya tano ya njano Januari Mosi, kwani Desemba 31, FA hawajaijumuisha.

Wakati huo huo, kuna kundi kubwa la wachezaji wa Ligi Kuu ambao wanatumikia adhabu za kadi tano za njano au nyekundu.

Marcos Alonso (Chelsea), Shane Duffy (Brighton), Christian Benteke (Palace), Jonathan Hogg (Huddersfield) na Wilfried Ndidi na Abdoulaye Doucoure wa Watford.

Jojo Shelvey ana adhabu ya kutocheza mechi mbili, huku Troy Deeney na Marvin Zeegelaar wote wa Watford wakiwa na adhabu ya kutocheza mechi tatu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU