SHAVU LA VANESSA MDEE UNIVERSAL MUSIC USIPIME

SHAVU LA VANESSA MDEE UNIVERSAL MUSIC USIPIME

469
0
KUSHIRIKI
NA CHRISTOPHER MSEKENA

NYOTA wa  Bongo Fleva, Vanessa Mdee, amesema dili lake jipya na lebo ya Universal Music Group kwa ushirikiano na Universal Music Germany na Airforce 1, itazidi kuupeleka mbali muziki wa Tanzania kwa kuwa yeye ndiye msanii pekee Afrika mwenye bahati hiyo.

Vee Money ameliambia Papaso la Burudani kuwa lebo ya Universal Music Group ni kubwa duniani, ina matawi ya Universal Music Africa ambayo inamsimamia Diamond Platnumz, Universal Music Europe, Universal Music America pamoja na Universal Music Central Europe ambayo anafanya nayo kazi hivi sasa.

“Nimesaini dili na Universal Music Central Europe pamoja na Afrika, ndiyo maana nimesema hili ni dili la kipekee kwa kuwa nimekuwa msanii wa kwanza Afrika kusaini dili la namna hii, nimesaini mwezi wa tano na hivi karibuni mashabiki wataanza kuona kazi zangu ikiwa ni pamoja na albamu itakayotoka mwezi wa sita chini ya Universal Music lakini pia ‘soon’ nitatoa albamu yangu ya Afrika (Money Mondays),” alisema Vanessa Mdee.

Aliongeza kuwa Air Force 1 ni lebo mpya ambayo kwa muda mrefu ilikuwa inatafuta msanii kutoka Afrika na bosi wa lebo hiyo alimtafuta ambapo ilichukua muda wa miezi sita ya mazungumzo mpaka kufikia makubaliano ya kufanya nao kazi ya kusambaza albamu na kazi zake nyingine.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU