MWAKA HUU UWE WA MAFANIKIO KATIKA MICHEZO

MWAKA HUU UWE WA MAFANIKIO KATIKA MICHEZO

163
0
KUSHIRIKI

KWANZA Bingwa tunatoa pole kwa familia ya marehemu Justine Limonga, mwandishi wa habari na mtangazaji nguli wa kipindi cha michezo za redio  Uhuru aliyefariki dunia jana, Dar es Salaam.

Tumesikitika kwa kifo cha ghafla cha mwandishi mwenzetu Limonga, aliyeshindwa kuona mwaka mpya wa 2018, lakini tunasema kazi ya Mungu haina makosa.

Sisi BINGWA tunasema kwamba, kifo cha Limonga kimetuacha njia panda kwa kuwa tumeondokewa na mtangazaji nguli katika vipindi vya mchezo na hatutasikia sauti yake tena, Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Ameen.

Tukiwa katika majonzi mazito ya kifo cha mwenzetu, tunawatakia heri ya mwaka mpya wote waliofanikiwa kuvuka na kuuona mwaka  wa 2018, lakini tunatoa pole kwa waliopata matatizo mbalimbali, wagonjwa ambao wako hospitalini wapone haraka.

BINGWA tunaukaribisha mwaka mpya kwa heri na fanaka, huku tukitarajia kuona sekta ya  michezo ikipiga hatua kubwa zaidi tofauti na miaka ya nyuma.

Tunasema hivyo tukijua kwamba mwaka huu, kutakuwa na mashindano mbalimbali ikiwamo michezo ya Jumuiya ya Madola iliyopangwa kufanyika Aprili mwaka huu, Mji wa Gold Coast nchi Australia.

BINGWA tanatarajia kuona timu zinakazoiwakilisha nchi katika michezo hiyo  ikiwamo ya riadha, kuogelea, meza, ngumi na paralimpiki zinafanya vizuri na kurejea na medali.

Tunaamini  kwamba, mwaka huu utakuwa wa neema kwetu  kutokana na maandalizi yanayoendelea kufanywa na wanamichezo wetu kwa ajili ya kushiriki Madola.

Pia tunatarajia kuona  mapinduzi makubwa ya soka baada ya Simba kupitisha mfumo wa uendeshaji wa klabu yao kwa kuuza hisa baadala ya wanachama kuendesha wenyewe kwa asilimia 100.

Kupitia mfumo huu, tunatarajia kuona  mafanikio makubwa katika soka kwa kuwa klabu nyingine zitafuata  mfumo ulioanzishwa na Simba.

Lakini ni mwaka ambao Simba na Yanga zitashirikisha michuano ya kimataifa, hivyo tunatarajia kuona zikifika mbali zaidi na mojawapo kama si wote kuchukua ubingwa wa Afrika.

BINGWA tunataka kuona  mafanikio makubwa  zaidi katika tasnia ya sanaa, tukiamini kwamba mwaka jana baadhi ya wasanii walifanya vizuri kitaifa na kimataifa.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU