LYYN: MASHABIKI WA ZARI WALIFANYA NIUCHUKIE UMAARUFU

LYYN: MASHABIKI WA ZARI WALIFANYA NIUCHUKIE UMAARUFU

289
0
KUSHIRIKI

KARIBU msomaji wa safu hii inayokupa nafasi ya kuwauliza maswali mastaa uwapendao nao wanakujibu hapa hapa bila chenga, kwa kufungua mwaka 2018, nimeona si jambo baya nikusogezee mahojiano niliyofanya na mrembo aliyetikisa tasnia ya burudani mwaka jana anayeitwa Irene au Lyyn, ambaye ni video queen aliyenogesha video mbili za Rayvanny, Kwetu na Natafuta Kiki upate kumfahamu zaidi.

SWALI: Ni kweli ulikataa kufanya video ya Abdul Kiba kwa sababu ya malipo madogo na ukakubali kufanya video ya Kwetu ya Rayvanny?

Irene: Sikukataa kwa ajili ya malipo ila Abdu Kiba aliponitafuta nilikuwa tayari nimefanya video ya Kwetu, kwa hiyo nisingeweza kufanya video nyingine kabla ile ya kwanza haijatoka, ilibidi nimwambie haiwezekani japo sikumwambia kwa sababu gani ndiyo maana akaona kama nimekataa.

SWALI: Umefanya video mbili tu lakini umekuwa mtu wa kusafiri sana nje ya nchi, unakula bata kwenye hoteli za kifahari nk, nani yupo nyuma ya hayo yote?

Irene: Binafsi napenda sana kusafiri na huko kote huwa naenda na boy friend wangu ambaye si mtu maarufu ndiyo huwa anasimamia kila kitu huko nje ya nchi tunakokwenda.

SWALI: Kwanini mavideo vixen wengi huwa mnaonekana wahuni?

Irene: Hiyo inatokana na baadhi yetu kufanya hayo mambo lakini si wote, wengine sisi tunaangalia kazi tu.

SWALI: Ulipata vipi nafasi ya kufanya video mbili za Rayvanny?

Irene: Nilikuwa natamani kufanya video za muziki, lakini sikuwa na njia, namshukuru Rayvanny yeye mwenyewe alinitafuta DM kwenye Instagram yangu, akaniomba kufanya video yake ya Kwetu, nilikaa kama siku tatu hivi tukakutana na kupanga namna ya kufanya, ikawa hivyo. Na kwenye Natafuta Kiki nilikuwa tayari nimezoea haikunisumbua sana.

SWALI: Ni vitu gani huwa unaangalia kwa mvulana?

Irene: Awe ana akili, anipende kweli na si lazima awe na fedha nyingi sana.

SWALI: Ni kweli uliwahi kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz mpaka ukashika ujauzito wake na ukautoa?

Irene: Hapana sikuwahi kutoka na Diamond na ile mimba ilikuwa ya boy friend wangu na bahati mbaya iliharibika.

SWALI: Kipindi hicho mashabiki wa Zari walikuandama sana, unaweza kuelezea ulikuwa kwenye wakati gani?

Irene: Sikujisikia vizuri sana, walikuwa wananichanganya nilikosa raha na nikatamani bora nisingefanya video ya Kwetu na nisingekuwa maarufu mpaka nikawaza nifute picha za Diamond zote ili nijiweke mbali naye.

SWALI: Kwanini huonekani kwenye video za wasanii wengine?

Irene: Wasanii wengi wananitafuta lakini tunatofautiana kwenye suala la malipo, hapo ndio tunashindwana ndiyo maana hunioni sana kwenye video ila mwaka 2018 kazi nyingi zitakuja.

Tuma swali lako kwa mwigizaji Tausi na Dj D Ommy, kupitia namba hapo juu, meseji tu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU