BARCA YA 2018 INAKUJA KWA ‘STYLE’ HII

BARCA YA 2018 INAKUJA KWA ‘STYLE’ HII

528
0
KUSHIRIKI

CATALUNYA, Hispania

HATIMAYE kikosi cha Barca kimerejea mazoezini baada ya mapumziko ya Mwaka Mpya.

Kwa mara ya kwanza tangu walipoichapa Real Madrid mabao 3-0, mastaa Lionel Messi, Luis Suarez na Javier Mascherano wameungana.

Messi na Suraez wameshafunga mabao jumla ya 25 na kuifanya Barca ikae kileleni mwa msimamo wa La Liga, ikiwa imewaacha kwa pointi 14 mahasimu wao Real Madrid.

Hata hivyo, huenda Mascherano akatimkia China hapo baadaye ikizingatiwa kuwa tayari ameshaanza mazungumzo na mabosi wa klabu ya Fortune Hebei.

Hiyo itawafanya Barca kutumia dirisha la usajili kumchukua beki mpya wa kati na kuna tetesi kuwa ni Yerry Mina wa Palmeiras.

Wakati huo huo, bado wanaifukuzia saini ya nyota wa Liverpool, Philippe Coutinho, licha ya kwamba hawataweza klumtumia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Habari za nje kwa wababe hao wa Catalunya ni kwamba, Ousmane Dembele anakaribia kupona majeraha yake.

Lakini pia, kuna tetesi kuwa tayari Barca wameanza kujipanga kuwapa mikataba mipya mastaa wake, Sergi Roberto na Gerard Pique na Samuel Umtiti ambaye klabu kadhaa zinamfukuzia.

Kwa upande mwingine, Rais wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu, anahangaikia mpango wa kumpa mkataba mpya mkurugenzi wake, Roberto Fernandez.

Tatizo jingine ambalo Bartomeu amepanga kulifanyia kazi mwaka huu ni kuongeza idadi ya watazamaji wanaofika Camp Nou, ambapo inaelezwa kuwa idadi imeshuka katika miaka ya hivi karibuni.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU