UNAMJUA ‘DOGO’ HUYU MAN CITY ALIYEONGEA KISWAHILI KRISMASI?

UNAMJUA ‘DOGO’ HUYU MAN CITY ALIYEONGEA KISWAHILI KRISMASI?

1581
0
KUSHIRIKI

MANCHESTER, England

HUENDA mashabiki wengi wanaoifuatilia Ligi Kuu England hawamjui Bryaydon Bent.  ‘Dogo’ mwenye umri wa miaka saba ambaye ni shabiki mkubwa  wa Manchester City.

Jina lake lilianza kuzungumziwa katika uliwengu wa soka Machi mwaka jana, baada ya kuposti ‘video’ iliyomuonesha akishangilia kama Sergio Aguero alipofunga bao dhidi ya QPR.

Kuanzia kipindi hicho, Bent amekuwa akifahamika ulimwenguni kote kuwa ni ‘shabiki damu’ wa timu hiyo ya jijini Manchester na amekuwa akifika uwanjani kuitazama.

Aguero amtafuta

Baada ya video hiyo iliyotazamwa zaidi ya mara 486,000, straika Aguero alimsaka na kukutana na ‘chalii’ huyo. Bent na Aguero walikutana kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Man City na Real Madrid.

Zaidi ya watu 6,000 ‘wali-like’   picha ya wawili hao katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

Baadaye, dogo huyo alikutana na kupiga picha na mastaa Willy Caballero, Kevin de Bruyne na Fernandinho.

Akutana na Guardiola, amtaka amchukue Messi

Julai mwaka jana, kwa mara ya kwanza Bent alikutana ana kwa ana na kocha wa Man City, Pep Guardiola, baada ya kupanda ‘taxi’  aliyokuwemo kocha huyo.

“Ni wewe?” Bent alimuuliza Guardiola ambaye hata hivyo hakuwa mchangamfu kutokana na kutomjua ‘dogo’ huyo.

Katika maongezi yao, Bent alimwomba Guardiola kumsajili staa wa Barcelona, Lionel Messi. Lakini pia, alimtaka kocha huyo kufika anakoishi ambako ni Cheshire.

Ampa keki Gundogan

Oktoba 24, mwaka 2016, kiungo wa Man City, Ilkay Gundogan, alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘birthday’.

Mbali na zawadi za mashabiki na wachezaji wenzake, Bent naye alijitokeza. Bent aligharamia keki na kumkabidhi nyota huyo wa zamani wa Borussia Dortmund.

Man City wampeleka Marekani

Kutokana na mapenzi yake kwa Man City, Bent alipata ‘shavu’ la kwenda kujirusha Marekani, gharama zote zikisimamiwa na na timu hiyo.

“Ilikuwa kama ndoto. Amekuwa kama balozi wa wachezaji chipukizi, hivyo Man City waliamua kumpa safari ya Marekani,” alisema mama yake Bent, Lorna Bent.

Azungumza Kiswahili

Ni moja ya matukio yake ya hivi karibuni. Bent alitumia mitandao ya kijamii kuwatakia mashabiki wake heri ya Sikukuu ya Krismasi na ndipo alipotamka kwa Kiswahili: “Mambo vipi?”

Akimzungumzia Bent, baba yake mzazi, Dad Mark alisema: “Tunafurahia. Man City wamekuwa wakimjali Braydon na tuna bahati kwa hilo.”

T

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU