NIYONZIMA AUMIA, KUKOSA MAPINDUZI

NIYONZIMA AUMIA, KUKOSA MAPINDUZI

1038
0
KUSHIRIKI

NA ZAINAB IDDY

KIUNGO wa timu ya Simba, Haruna Niyonzima, amesema kitendo cha kushindwa kuitumikia timu hiyo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kinamuumiza, lakini ataendelea kukiombea kikosi hicho kipate mafanikio.

Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi Desemba 29, mwaka jana visiwani Zanzibar, ambapo Simba ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mwenge katika mchezo wake wa kwanza.

Niyonzima ameshindwa kuambatana na kikosi cha Simba kinachonolewa na kocha Masoud Djuma raia wa Rwanda, kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.

Akizungumza na BINGWA, Niyonzima, alisema anafahamu timu yake ina wachezaji wazuri na wanaotambua majukumu yao lakini kama angekuwepo angeongeza nguvu.

“Simba ina wachezaji wenye uwezo wa kuleta chachu ya ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, lakini naamini ningekuwepo ningeongeza kitu cha ziada ambacho kingetupa mafanikio.

“Lakini kwa kuwa Mungu hakupanga niwe na timu, nimelazimika kubaki jijini Dar es Salaam kuendelea na matibabu ya kifundo cha mguu.

“Hivyo sina budi kuwaombea afya njema wachezaji wenzangu waliopo kwenye timu ili wapambane na kurejea na taji la ubingwa,” alisema Niyonzima.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU