CONTE AWAKOROMEA MABOSI CHELSEA

CONTE AWAKOROMEA MABOSI CHELSEA

242
0
KUSHIRIKI
LONDON, England

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte, amegeuka mbogo na tayari ameshaweka wazi kuwa hafurahishwi na utendaji kazi wa mabosi wanaohusika katika usajili wa wachezaji klabuni hapo.

Muitalia huyo amesema kinachomkera zaidi ni kwamba, hajashushiwa wachezaji anaowataka, ambao anaamini akipewa ataifanya Chelsea kuwa tishio Ligi Kuu England. “Ni mara chache nimekuwa nikipewa wachezaji niliowataka,” alisema.

Conte aliyasema hayo baada ya mchezo wake dhidi ya Arsenal juzi ambapo kikosi chake kilitoka sare ya mabao 2-2.

Tangu alipoanza kukinoa kikosi hicho cha Magharibi mwa Jiji la London, Conte, ameshasajili wachezaji 11, akitumia kitita cha pauni milioni 297.5.

Katika dirisha la usajili la mwezi huu, mkufunzi huyo amekuwa akimtolea macho kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal, ambaye hata kumnasa kwake atalazimika kuweka mezani zaidi ya pauni milioni 30.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU