ESSIEN AJENGEWA SANAMU GHANA

ESSIEN AJENGEWA SANAMU GHANA

200
0
KUSHIRIKI
ACCRA, Ghana

KIUNGO wa kimataifa wa Ghana, Michael Essien, amepewa heshima ya kujengewa sanamu nchini humo.

Kama ilivyowahi kutokea kwa mastaa Cristiano Ronaldo na Diego Maradona, ambao pia wamefanyiwa hivyo kwao, sanamu la Essien litakuwa jijini Accra.

Essien mwenye umri wa miaka 35, aliichezea Ghana mechi 58 na pia alikuwa na Chelsea kwa miaka tisa.

Kwa kipindi hicho alichokaa Stamford Bridge, alishinda vikombe viwili vya Ligi Kuu England, vinne vya Kombe la FA na kimoja cha Kombe la Ligi.

Mbali na Blues, pia alizichezea AC Milan na Panathinkaikos na sasa anaichezea Persib Bandung ya Indonesia.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU