GIOVANNI AMTABIRIA SIMEONE KUREJEA INTER MILAN

GIOVANNI AMTABIRIA SIMEONE KUREJEA INTER MILAN

156
0
KUSHIRIKI
ROMA, Italia

STRAIKA wa Fiorentina, Giovanni, amsema kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone, atarejea kuinoa Inter  Milan kipindi kifupi kijacho.

Kauli ya staa huyo imekuja zikiwa ni siku chache tangu Simeone ambaye ana mkataba wa kuinoa klabu hiyo ya  Wanda Metropolitano hadi mwaka 2020 kuweka wazi ndoto zake za kuinoa Inter  Milan ambayo aliwahi kuichezea.

Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 47 ambaye alikaa nchini Italia kwa kipindi cha miaka miwili, aliiwezesha Inter kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa msimu wa 1997-98.

Giovanni ambaye mara kadhaa amekuwa akimzungumzia Diego na matarajio yake ya kurejea Inter Milan, amerudia tena kauli hiyo kabla ya mechi ya leo ya  Fiorentina dhidi ya kigogo hicho.

“Nadhani kuna wakati utafika,” Giovanni aliuambia mtandao wa Premium Sport.

“Kwa sasa anafurahi akiwa Atletico, lakini siku moja atakuja,” aliongeza nyota huyo.

Mpaka sasa Simeone ameshatwaa ubingwa wa La Liga na Ligi ya Europa na mara mbili ameshashika nafasi ya pili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa tangu alipoichukua timu hiyo mwaka 2011.

Atletico inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga na ipo nyuma kwa pointi nane dhdi ya vinara wanaoongoza ligi hiyo, Barcelona ikiwa imecheza mechi 17.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU