KOCHA KUIDAKIA BAYERN KISA MAJERAHA

KOCHA KUIDAKIA BAYERN KISA MAJERAHA

853
0
KUSHIRIKI
MUNICH, Ujerumani

ALIYEWAHI kufanya kazi ya kuwanoa makipa wa Bayern Munich, Tom Starke, atalazimika kukaa langoni baada ya kikosi hicho kuwapoteza walinda mlango wake wawili kutokana na majeraha.

Baada ya Manuel Neuer kuwa nje kwa muda mrefu, Bayern watamkosa pia mrithi wake, Sven Ulreich, ambaye naye aliumia akiwa mazoezini jijini Doha, Qatar.

Hivyo, sasa Bayern watamgeukia Starke ambaye alistaafu wakati wa majira ya kiangazi yaliyopita, kabla ya kurudi baada ya mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya Ujerumani kuwa majeruhi.

Kesho Bayern watashuka dimbani kumenyana na Al Ahly, mchezo utakaochezwa Qatar, kabla ya kuwafuata Bayern Leverkusen katika mtangane wa Bundesliga utakaopigwa Januari 12.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU