MAYWEATHER: NATAKA MPUNGA TU 2018

MAYWEATHER: NATAKA MPUNGA TU 2018

214
0
KUSHIRIKI
LOS ANGELES, Marekani

BONDIA Floyd Mayweather amefichua mipango yake ya mwaka huu akisema ni kutengeneza fedha tu.

Mayweather mwenye umri wa miaka 40, alidai kuwa anataka kuutumia mwaka 2018 kuongeza kiasi chake cha fedha kilichopo benki.

“Kila mtu anasema ‘Heri ya Mwaka Mpya’…Mimi napenda kupata fedha mpya kila mwaka!” aliandika Mayweather katika ukurasa wake wa Instagram.

Kabla ya pambano lake dhidi ya Conor McGregor mwaka jana, supastaa huyo alikuwa anatajwa kuwa na utajiri wa Dola milioni 700 (zaidi ya Sh trilioni moja za Tanzania).

Kwa sasa Mayweather hafanyi kazi chini ya Kampuni ya Top Rank ambayo inamilikiwa na promota maarufu, Bob Arum.

“Katika mambo ya ajabu ambayo nimewahi kuyafanya ni kusaini kuwa chini ya Top Rank,” alisema Mayweather alipokuwa akihojiwa na mtandao wa FightHype.

Ingawa hakutaja jina, Mayweather alisema mmoja kati ya mabosi wa kampuni hiyo ana njaa ya fedha na alikuwa ‘akimpiga’ katika malipo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU