WALCOTT ALILIA KUKIPIGA MILAN

WALCOTT ALILIA KUKIPIGA MILAN

148
0
KUSHIRIKI
LONDON, England

ILI kukinusuru kiwango chake ambacho kinaelekea kuuliwa na benchi pale Arsenal, Theo Walcott, ameamua kuwaita AC Milan wamchukue.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, hajaingia ‘first eleven’ tangu kuanza kwa msimu huu.

Licha ya kutakiwa na klabu za Southampton, Everton na West Ham, mshambuliaji huyo amesema angependa kwenda nje ya England.

Gazeti moja la Italia lilisema tayari Milan nao wanaangalia uwezekano wa kumchukua kwa mkopo wa miezi sita.

Hata hivyo, Milan hawataweza kumtumia Walcott kwenye Ligi ya Europa kwa kuwa tayari ameshaiwakilisha Arsenal katika michuano hiyo msimu huu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU