WENGER AMPIGIA DEBE WILSHERE KIKOSI ENGLAND

WENGER AMPIGIA DEBE WILSHERE KIKOSI ENGLAND

113
0
KUSHIRIKI
LONDON, England

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amekisifia kiwango kilichooneshwa na nyota wake, Jack Wilshere na akasema kwamba anavyoonekana yupo fiti hata kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya England.

Kauli hiyo ya Wenger imekuja baada ya  usiku wa kuamkia jana Wilshere kufunga bao lake la kwanza katika michuano ya Ligi Kuu England tangu Mei 2015 na la kwanza katika mchezo ambao Arsenal walitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya  Chelsea.

Msimu huu kiungo huyo ameshacheza michezo 11, lakini kati ya hiyo ni sita tu ambayo alianza kikosi cha kwanza.

Mechi ya mwisho kwa Wilshere kuchezea timu ya Taifa ya England ilikuwa ni wakati wa fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2016, lakini  Wenger anasema kwamba haitashangaza  kama ataitwa kwenye kikosi hicho ambacho kinajiandaa na fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika miezi mitano ijayo nchini Urusi.

“Kwa sasa yupo katika kiwango ambacho watu wengi hawakutarajia atakuwapo,” Wenger aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

“Nakumbuka kwa mara ya mwisho kuichezea England ilikuwa ni dhdi ya  Iceland katika fainali za Euro 2016 na alifanya vizuri. Tangu kipindi hicho hajawahi kuichezea England na ninachoweza kusema kila mmoja ameshampotezea. Ila kwa leo haitashangaza kama ataitwa tena,” aliongeza kocha huyo.

Kwa sasa Arsenal wanashika nafasi ya  sita kwenye msimamo wa ligi wakiwa nyuma kwa pointi tano dhidi ya Liverpool ambao wanashika nafasi ya nne.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU