HUYU NDIYE KONSTANTINOS MAVROPANOS USIYEMJUA

HUYU NDIYE KONSTANTINOS MAVROPANOS USIYEMJUA

532
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

WASHIKA mitutu wa London, Arsenal, wamekamilisha dili la kumsajili beki wa Kigiriki, Konstantinos Mavropanos, kutoka PAS Giannina, lakini beki huyo wa kati ni nani hasa?

Ugiriki wanamchukuliaje?

Nchini kwao wanafurahishwa mno na kipaji chake hasa kutokana na udogo wake kiumri na umaarufu wake wa ghafla unafananishwa na Panagiotis Retsos, kinda la miaka 19 aliyevunja rekodi ya usajili Ugiriki kwa kusajiliwa na Leverkusen kutoka Olympiakos.

Mavropanos ameisaidia sana klabu ya PAS katika Ligi Kuu Ugiriki, timu ambayo bado ni ndogo lakini amefanikiwa kutengeneza jina lake hapo.

Kiwango chake kilizichanganya timu nyingine kama vile AEK Athens kabla ya kuajiriwa na Arsenal.

 

Ni ajabu Arsenal kumsajili?

Licha ya Mavropanos kuibuka kwa kasi, inashangaza Arsenal kumsajili kwani ni mchezaji ambaye amecheza kwenye mechi mbili tu za Ligi Kuu ya Ugiriki.

Hata kufananishwa na Retsos nako kunashangaza kwani, Retsos alifukuziwa sana mwaka mmoja kabla na tayari alishaanza kuitwa timu ya taifa na alijulikana kuliko Mavropanos, uzoefu pia alikuwa nao wa kutosha.

Kinda huyo alianza kufukuziwa na timu kubwa miezi miwili tu iliyopita hivyo kitendo cha Arsenal kumkimbilia mapema kinashtusha.

Nguvu na udhaifu

Nguvu kubwa ya Mavropanos ni kupokonya mipira kutoka kwa adui na kucheza mipira ya juu. Futi zake 6 na inchi 4 zitamsaidia sana England huku akiwa ni mfungaji mzuri pia (mabao matatu msimu huu akiwa PAS).

Beki huyo ana nguvu sana. Hana makosa ya mara kwa mara kwenye kumiliki mpira au kukaba ana kwa ana. Ni mpole na msikilizaji mzuri sana na tangu akiwa mdogo alionesha wazi anataka kuwa kiongozi wa kuigwa uwanjani.

Kiufundi, Mavropanos si mchezaji mbaya ingawa anatakiwa kuboresha kiwango chake kwa ajili ya kuzoea soka la England. Atatakiwa kuwa na mguso bora wa kwanza wa mpira na kuumiliki kwa kujiamini kwani atakutana na mashambulizi makali mno kwani ligi aliyotoka na aliyotua kwa sasa ni tofauti kabisa.

 

Ataimarika kwa kiasi gani?

Anaonekana kuwa mzuri kimwili na kiakili katika harakati zake za kuwa mchezaji bora na anasubiriwa kuonekana kama atafanikiwa kufanya hivyo England na katika klabu ya Arsenal.

Hata hivyo, beki huyo ana uwezo pia wa kufikia hadhi ya mabeki wa Kigiriki wanaotesa kwa sasa; Sokratis Papastathopoulos wa Borussia Dortmund na Kostas Manolas wa Roma, kinachohitajika ni uzoefu tu.

Hana uhakika wa nafasi kikosi cha kwanza Arsenal, lakini kwa kuwa atatolewa kwa mkopo, ana uwezo wa kuja kushindania nafasi hapo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU