NI KISASI SIMBA, AZAM KOMBE LA MAPINDUZI

NI KISASI SIMBA, AZAM KOMBE LA MAPINDUZI

787
0
KUSHIRIKI

NA JESSCA NANGAWE

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi timu ya Azam FC, leo itashuka dimbani kuvaana na Simba kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, ukiwa ni mwendelezo wa michuano hiyo inayoendelea visiwani humo.

Simba na Azam ambazo zimezoeleka kuwa na ushindani mkubwa pale zinapokutana, zitatumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yao ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo kwa sasa imesimama kwa muda.

Azam ambayo imeshinda michezo miwili, jana ilikuwa ikivaana na URA na kama watakuwa wameshinda, watakuwa wametinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Kwa upande wa Simba ambao wana pointi nne, walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Mwenge kwenye mchezo wao wa kwanza kabla ya juzi kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jamhuri.

Kocha wa Azam, Aristica Ciaoba, amesema licha ya ratiba ya michuano hiyo kuwabana, lakini hawana tatizo lolote kwa kuwa lengo lao ni kuona wanafanya vyema kwenye michuano hiyo ili waweze kutetea ubingwa wao sambamba na kufanya vyema kwenye ligi kuu.

 

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU