UMEUONA UMAFIA WA BARCA KWA COUTINHO

UMEUONA UMAFIA WA BARCA KWA COUTINHO

758
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

KABLA ya kuendelea, ieleweke kwamba makala hii haisemi kwamba klabu ya Barcelona inamshawishi kiungo, Philippe Coutinho, aiache timu yake ya Liver na kutua Camp Nou.

Hiyo ni kinyume na sheria za Shirikisho la Soka Duniani (Fifa).

Ni zaidi ya mwaka sasa tangu Coutinho aanze kuhusishwa na Barcelona. Sekeseke lake limepata ‘kiki’ kuliko Dk. Shika na sasa limerudi upya Januari hii.

Kama hiyo haitoshi, mtandao wa kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Nike, tayari imemtaja Coutinho kama mchezaji wa Barca, mashabiki wa Liverpool wanasali nyota wao asiondoke na wamiliki wa ‘The Reds’ wapo bize kuzikataa ofa zote zitakazokuja mezani.

Lakini, Liverpool haitokuwa timu ya kwanza kushuhudia nyota wake akienda Nou Camp na haitokuwa timu ya mwisho. Barca wana mbinu kali mno za kushawishi wachezaji na huwa hawaogopi.

Mashabiki wa Arsenal watakumbuka kuhusu Thierry Henry na Cesc Fabregas. Wale wa Liverpool bado wanamkumbuka Luis Suarez.

Hizi sasa ndizo njia saba wanazotumia Barcelona hadi kumpata mchezaji wanayemtaka.

 

1: Mtafute, yuko wapi?

Hii ni kazi ngumu kwa Barca, kuanza kuwasiliana na maskauti duniani kote, watumie saa nyingi sana kuwachambua na kutambua yupi ana kipaji na atakayeingia kwenye falsafa yao moja kwa moja.

Wanapomgundua tu, basi hawezi kuchomoka kwenye mitego yao. Kwa miaka ya hivi karibuni, Barca ni nadra kusikia ikikataliwa na mchezaji nyota. Nani atakataa fursa ya kucheza na Lionel Messi mbele ya mashabiki 98,000?

Mipango yao ni kumpata nyota wa Kibrazil atakayechukua nafasi ya Neymar na awasaidie kibiashara kwani walishapoteza mtaji wa mashabiki kutoka Brazil baada ya staa huyo kuhamia PSG. Kazi ya maskauti ishaisha, wameshajua nani atakayewafaa.

 

2: Tafuta wa kumshawishi

Njia ya pili ni kuwapanga wachezaji watakaoweza ‘kumtongoza’ mchezaji akubali kutua Camp Nou, kwenye hili eneo, Coutinho ataambiwa kuhamia Barca litakuwa jambo jema zaidi katika maisha yake ya soka.

Nani watahusika kumjaza maneno?

Luis Suarez atafaa. Mbrazil mwenzake,  Paulinho, pia atahusika. Barca pia watamtumia mkongwe anayeheshimika Camp Nou, Xavi Hernandez. Halafu watamalizia kumwomba mkongwe wa zamani wa Brazil, Rivaldo, naye amshawishi Coutinho aondoke Anfield.

 

3: Anzeni kumshawishi

Baada ya kupata watu wa kumshawishi, kazi sasa inaanza. Suarez atamkumbushia Coutinho jinsi walivyokuwa na furaha pamoja Anfield. Paulinho atamkumbusha Coutinho jinsi walivyokua pamoja utotoni na atafurahi sana kusikia anatua Camp Nou.

Xavi naye atasema: “Hakuna wachezaji wengi sana wenye uwezo wa kuiboresha Barcelona lakini ukiniuliza kama atafaa, nitakukubalia.”

 

4: Ibuka na ofa ghafla

Hapa lazima Coutinho alegee tu. Ni rahisi sana kudharau tetesi lakini si ofa ya maana, tena ile iliyochapishwa kwenye magazeti.

Agosti, 2017, Barca walijua wasingeweza kumpata Coutinho kwa pauni milioni 72 lakini walipanga kumfanya kiungo huyo afikirie kuhusu uhamisho muda wote.

Lazima mchezaji avurugike kiakili na kuomba auzwe, kama ilivyokuwa kwa Coutinho. Na akikataliwa ombi lake lazima atajisikia vibaya na kuamua kuomba tena auzwe hadi atakapokubaliwa.

 

5: Jezi

Unakumbuka jinsi Fabregas alipovishwa jezi ya Barca mwaka 2010, baada ya Hispania kutwaa Kombe la Dunia? Siku chache baadaye akaondoka Arsenal.

Katika kipindi hiki, tegemea kuona Coutinho akivishwa jezi na Paulinho!

 

6: Hakikisha magazeti ya Katalunya yanachochea

Kwa Barcelona, magazeti ya Sport na Mundo Deportivo ndiyo silaha zao na huwa hayakosi habari muhimu za Barca hata siku moja.

Ukiingia kwenye mitandao yao lazima ukute habari nyingi za Coutinho kuanzia mishahara yao huko waliko, mikataba yao inaisha lini, watachezaje au kabati lake la kubadili nguo litakuwaje.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU