UMESIKIA?

UMESIKIA?

583
0
KUSHIRIKI

LONDON, England


th (1)

KUNA jambo kubwa linaendelea baina ya makocha wawili, Antonio Conte na Jose Mourinho na sasa limepamba moto.

Kocha wa Man United, Mourinho ndiye aliyeanza uchokozi kwa kukumbushia skendo ya kupanga matokeo iliyowahi kumkumba Conte, ambapo kocha huyo wa Chelsea hakupendezwa na maneno hayo, baada ya vijana wake kushinda mabao 2-0 dhidi ya Derby County kwenye mchezo wa FA.

Katika kuhakikisha na yeye haonekani mzembe, Conte alijibu mapigo kwa kusema Mourinho ni ‘mtoto’ na ‘asiye na uhalisia’, wikiendi iliyopita baada ya kumalizika kwa mchezo wa timu yake dhidi ya Norwich.

Conte alikumbwa na adhabu ya kufungiwa mechi nne katika msimu wa 2012-13, baada ya kushindwa kuwasilisha ripoti yake juu ya skendo ya kupanga matokeo alipokuwa kocha wa Siena, lakini mwaka 2016 alifutiwa tuhuma hizo.

“Mourinho namuona kama mtoto, unajua kabla ya kuzungumza haya mambo ni lazima ujue ukweli kwanza.

“Inabidi uwe makini sana kwani ni kauli za kuumiza moyo wa mtu. Ukikosa umakini na kuzungumza kabla ya kuchunguza unaonekana kama mtoto. Namjua Mourinho tangu zamani, utoto wake hajauanza leo na anaonekana wazi hatabadilika.

“Mourinho si tatizo kwangu. Nakumbuka aliwahi kuzozana na Claudio Ranieri. Kisa ni Ranieri hajui kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha, Ranieri alipofukuzwa akavaa fulana yenye jina lake. Huo sasa ndiyo unafiki ninaouzungumzia.

“Unaanza ugomvi na mtu fulani na nia ya kumuua. Baada ya miaka miwili unajifanya kutaka kumsaidia ili ujipatie umaarufu.

“Namsubiri kwenye mechi kati ya timu yangu na yake pale Old Trafford. Uso kwa uso. Niko tayari, ila sidhani kama yeye amejiandaa,” alisema.

Man United na Chelsea zinatarajiwa kukutana Februari 25 kwenye mechi ya Ligi Kuu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU