CONTE AMPA KIBARUA BARKLEY

CONTE AMPA KIBARUA BARKLEY

520
0
KUSHIRIKI
LONDON, England

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte, ni kama amempa kibarua nyota wake, Ross Barkley, kuhakikisha anapata namba kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya England ambacho kitakwenda kushiriki fainali za Kombe la Dunia baadaye mwaka huu baada ya kuhamia Stamford Bridge.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 24, alikamilisha uhamisho wake Ijumaa wiki iliyopita akitokea Everton kwa ada ambayo inasemekana kuwa ni pauni milioni 15 licha ya kuwa ameshazikosa mechi zote za msimu huu kutokana na kukabiliwa na majeraha ya misuli ya nyama za paja.

Kwa mara ya mwisho, Barkley kuichezea nchi yake ilikuwa wakati wa mechi ya kirafiki ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Australia iliyopigwa Mei 2016, lakini Conte  ana matumaini msimu huu anaweza kuonesha kiwango ambacho kitamshawishi kocha wa England, Gareth Southgate.

“Tunazungumzia wachezaji wenye kipaji cha hali ya juu,” alisema kocha huyo.

“Kabla ya kuwa na majeraha haya mabaya alikuwa na timu ya taifa. Nadhani tuna miezi mitano ya kuonesha anafaa kuitwa katika timu ya taifa kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia. Nafikiri itakuwa hivyo kwa sababu atafanya vizuri akiwa nasi,” aliongeza kocha huyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU