COUTINHO KUKAA BENCHI WIKI TATU, ATAMBULISHWA KIAINA

COUTINHO KUKAA BENCHI WIKI TATU, ATAMBULISHWA KIAINA

250
0
KUSHIRIKI
MADRID, Hispania

TIMU ya Barcelona imethibitisha kuwa staa wao mpya ambaye wamemsajili kwa bei kubwa, Philippe Coutinho, hataweza kuichezea kwa sasa mpaka ifikapo mwishoni mwa mwezi huu kutokana na majeraha ya misuli ya nyama za paja yanayomkabili.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye juzi alikamilisha uhamisho wake wa kuhamia katika klabu hiyo vinara wa  La Liga kwa ada inayoripotiwa kuwa ni Euro milioni 160, alikuwa hajacheza tangu Desemba mwaka jana kutokana na maumivu ya tatizo hilo.

Nyota huyo raia wa Brazil ambaye pia alifuzu vipimo vya afya juzi hiyo, lakini ikabainika kuwa anatakiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa siku 20.

Kutokana na hali hiyo sasa Coutinho ataikosa mechi ya keshokutwa ya  michuano ya Kombe la Copa del Rey  dhidi ya Celta Vigo na za ligi dhidi ya  Real Sociedad na Real Betis.

Staa huyo atarejea mzigoni wakati timu hiyo itakaposafiri kwenda kuikabili  Deportivo Alaves Januari 28, mwaka huu na nyingine dhidi ya  Espanyol ambako mwaka 2012 alikuwa akikipiga kwa mkopo.

Coutinho ametambulishwa kama mchezaji wa Barcelona kwa mara ya kwanza.

Hata hivyo, tofauti na ilivyo kwa wachezaji wengine, Barca walifanya onesho hilo kwa namna ya kipekee kwenye video ambayo ilirushwa kupitia akaunti ya klabu ya Twitter baada ya ushindi wa juzi dhidi ya Levante.

Coutinho alioneshwa akitembea jukwaani akizitazama kamera, akiwapungia wapiga picha na kuwaonyesha alama ya dole gumba kwa ajili ya picha.

“Salamu Barcelona, tayari nipo hapa,” alisema Coutinho. “Ni ndoto iliyotimia na natumai tutaonana kesho.”

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU