MESSI AFIKIA REKODI YA GERD MULLER

MESSI AFIKIA REKODI YA GERD MULLER

245
0
KUSHIRIKI
MADRID, Hispania

STAA wa Barcelona, Lionel Messi, amefikia rekodi ya staa wa zamani, Gerd Muller, iliyodumu kwa muda mrefu kwa kuweka kimiani mabao 365 katika michuano ya La Liga akiwa na klabu yake ya Barcelona.

Mkali huyo raia wa Argentina, alifungua ukurasa wa mabao kwa miamba hao wa Catalan juzi, baada ya kupachika bao la  kiufundi dhidi ya Levante.

Kabla ya kupachika bao hilo, Messi aligongeana na mchezaji mwenzake mkongwe, Jordi Alba na kumalizia kwa kuukwamisha wavuni mpira kuipa goli la kuongoza 1-0 timu yake katika ushindi wa 3-0 ugenini.

Na kwa kufanya hivyo nyota huyo  alilingana mabao  na staa wa  zamani wa Bayern na Ujerumani, akiifikia rekodi ambayo imedumu kwa muda wa miaka 39.

Sasa amefunga mabao 365 akiwa Blaugrana katika mechi 400 za La Liga, akiifikia rekodi hiyo ya kihistoria ya Muller aliyofanikiwa kuiweka kwenye klabu moja miongoni mwa Ligi Kuu tano za Ulaya.

Rekodi inaweza kuvunjika Jumapili ijayo Barca watakapoitembelea Real Sociedad.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU