PAUNI MIL 35 KUMPELEKA OZIL MAN UTD

PAUNI MIL 35 KUMPELEKA OZIL MAN UTD

740
0
KUSHIRIKI
LONDON, England

TIMU ya Manchester United imesema kwamba, inaamini pauni milioni 35 zinatosha kumng’oa kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil, wakati wa usajili wa mwezi huu.

Ozil ambaye yupo kwenye mwaka wake wa mwisho, amegoma kuongeza mkataba mpya pale Emirates na gazeti la Mirror limesema kwamba, Mourinho amepewa ruksa ya kuzungumza na nyota huyo mwenye umri wa miaka 29.

Gazeti hilo pia limesema kwamba, Mourinho, amepanga kutumia pauni milioni 80 kwa mwezi huu wa Januari na anajiandaa kujadiliana na Gunners  kuhusu bei ya kulipa kwa ajili ya nyota huyo.

Wenger ana nia ya kumbakiza kwenye klabu hiyo ya Kaskazini mwa jiji la  London nyota huyo wa Ujerumani, licha ya Ozil kubakiza siku chache kwenye mkataba wake.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU