WEMA SEPETU APATA MTETEZI MPYA

WEMA SEPETU APATA MTETEZI MPYA

325
0
KUSHIRIKI

NA MWANDISHI WETU

KESI ya kutuumiwa kukutwa na kutumia dawa za kulevya inayomkabili msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, jana iliendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo wakili aliyekuwa anasimamia kesi hiyo, Peter Kibatala, aliandika barua ya kujitoa huku, Alberto Msando, akiandika barua ya kuwa wakili mpya wa kumtetea mrembo huyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, alisema amepokea barua za mawakili, Peter Kibatala na Alberto Msando, Januari 9, mwaka huu ambapo Kibatala aliomba kujitoa kumwakilisha, Wema Sepetu, kwenye kesi hiyo huku sababu za kujitoa hazikuwekwa wazi.

Pia Hakimu, Simba alisema katika barua ya wakili, Alberto Msando, aliomba kumtetea, Wema Sepetu, hivyo anaomba apewe muda wa kulisoma jalada la kesi hiyo ili aanze kumuwakilisha mrembo huyo mahakamani ambapo yeye (Hakimu Thomas Simba), alikubaliana na barua za mawakili wote wawili na kuahirisha kesi hiyo mpaka Februari 8, mwaka huu.

Mbali na Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambapo kwa pamoja wanashtakiwa kwa makosa mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya aina ya bangi pamoja na kutumia.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU