NYOSHI EL SADAAT AITABIRIA MAKUBWA BOGOSS MUSICA

NYOSHI EL SADAAT AITABIRIA MAKUBWA BOGOSS MUSICA

364
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya kujiweka pembeni ya Fm Academia, mwanamuziki mahiri wa dansi nchini, Nyoshi El Sadaat, ameitabiria makubwa bendi yake mpya inayoitwa, Bogoss Musica.

Rais huyo wa Bogoss Musica ambaye ameiongoza bendi ya Fm Academia kwa muda wa miaka 20, ameliambia Papaso la Burudani kuwa hivi sasa yeye na wanamuziki wake wapo chimbo wanajipanga kuja kutikisa tasnia ya muziki huo.

“Nguvu zangu nyingi kwa sasa zipo Bogoss Musica, tunaendelea kufanya mazoezi na kurekodi kazi mpya ambazo mashabiki wakae tayari kuzipokea mwezi ujao au wa tatu hivi tutaanza kuzitoa,” alisema Nyoshi.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU