SIMBA YAAMSHA HASIRA NDANDA

SIMBA YAAMSHA HASIRA NDANDA

934
0
KUSHIRIKI

NA TIMA SIKILO

KOCHA wa Ndanda, Hamsin Malale, amesema kipigo walichokipata kutoka kwa Simba kimeamsha hasira na sasa wanaendelea kujifua ili kuibuka na ushindi katika mchezo utakaofuata wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC.

Ndanda waliopoteza kwa Simba baada ya kufungwa mabao 2-0 katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa Desemba 30, mwaka jana kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara.

Akizungumza na BINGWA jana, Malale alisema baada ya kupoteza kwa Simba wanajipanga ili kuhakikisha hawapotezi  dhidi ya Mbao FC.

Malale alisema wachezaji wake wana morali ya hali ya juu kuhakikisha wanaifunga Mbao ili waweze kujiongezea pointi na kupanda nafasi moja zaidi katika msimamo wa ligi hiyo.

Alisema hawatakubali kuendelea kupoteza kwa kuwa utakuwa ni mchezo wa mwisho kucheza kwenye uwanja wao wa nyumbani katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

“Mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Simba tulipoteza, lakini umetupa morali ya kufanya vizuri katika mchezo wetu dhidi ya Mbao,” alisema Malale.

Katika hatua nyingine, mshambuliaji wa timu hiyo, Omar Mponda, amewataka mashabiki kutulia kwani kuna mambo mazuri yanakuja.

Mponda alisema wanaendelea kujifua ili waweze kufanya vizuri kwa michezo inayofuata.

Ndanda inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi  11 wakati Mbao ikiwa nafasi ya saba na pointi     14.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU