AJIB LAWAMANI PENALTI YA CHIRWA

AJIB LAWAMANI PENALTI YA CHIRWA

2070
0
KUSHIRIKI
NA SAADA SALIM, ZANZIBAR

PENALTI aliyoikosa Obrey Chirwa wa Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar dhidi ya URA ya Uganda juzi, imezua jambo ndani ya kikosi cha Wanajangwani hao ambapo imemwingiza matatani nyota wao, Ibrahim Ajib.

Chirwa alikosa penalti ya tano wakati wa hatua ya matuta baada ya timu hizo kutoka suluhu ndani ya dakika 90 za kawaida kwenye Uwanja wa Amaan.

Kitendo cha Chirwa kukosa mkwaju huo ulioing’oa Yanga, kimepokewa kwa hisia tofauti na wapenzi wa klabu hiyo, wengi wakihoji kulikoni Mzambia huyo kupewa nafasi ya kupiga penalti wakati akiwa na timu kwa muda mrefu baada ya kukimbilia kwao kwa kile kilichodaiwa kumuuguza mzazi wake.

Mshambuliaji huyo alijiunga na wenzake mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo hakuhusika katika mechi zote za awali za michuano hiyo ambapo Yanga haikupoteza mchezo hata mmoja kabla ya kutolewa na URA kwa mikwaju ya penalti 5-4 juzi.

Wanaompinga Chirwa wanaamini Mzambia huyo hakupaswa kupangwa katika mchezo wa juzi, ikiwamo kupiga penalti wakisisitiza kulikuwa na wachezaji wengi waliostahili kufanya hivyo, akiwamo Ajib ambaye ………………………….

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya BINGWA.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU