GERRARD AMBANIA ALONSO UKOCHA LIVERPOOL

GERRARD AMBANIA ALONSO UKOCHA LIVERPOOL

399
0
KUSHIRIKI
LONDON, England

MSHINDI wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Liverpool mwaka 2005, Xabi Alonso, amesema anatamani kuinoa timu hiyo miaka ijayo lakini anahisi Steven Gerrard atawahi kabla yake.

Alonso alifunguka wazi kuhusu nia yake hiyo alipokuwa akifanya mahojiano na mchambuzi wa soka wa kituo cha talkSPORT, Guillem Balague.

“Ni kweli, nina ndoto hai za kuwa kocha wa Liverpool. Kwanza ujue inabidi niwe na uhakika na kujiandaa,” alisema.

“Lakini sidhani kama nitawahi kabla ya Gerrard, yeye tayari ameshaingia pale na nahisi atawahi kuwa kocha mkuu kabla yangu.”

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU