MOURINHO APANIA KUIKATILI MAN CITY KWA SANCHEZ

MOURINHO APANIA KUIKATILI MAN CITY KWA SANCHEZ

479
0
KUSHIRIKI
MANCHESTER, England

USAJILI wa Januari umepamba moto ambapo klabu ya Manchester United imeripotiwa kuibuka na ofa nono kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, ambaye pia anawaniwa na wapinzani wao wa jadi, Man City.

City walitoa ofa ya pauni milioni 20 kumsajili Sanchez na dili lilionekana kukaribia kukamilika na Mchile huyo kuungana na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola, aliyeko Man City kwa sasa.

Lakini ripoti zilizoibuka jana zilidai kuwa United iliandaa ofa nzuri ambayo ilikaribia pauni milioni 35 wanazotaka Arsenal ili wamuuze Sanchez na kumtumia kiungo wao, Henrikh Mkhitaryan, kama moja ya makubaliano.

Ofa ambayo United walidaiwa kuitoa ni pauni milioni 25.

Inaaminika kwamba, Sanchez pamoja na kambi yake tayari wamekubaliana masuala binafsi na Man City ambayo itatoa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki lakini United imeibuka na kutamba kwamba wataweza kuwapiku wapinzani wao hao.

Usajili huo huenda ukasababishwa na presha ambayo Mourinho ameupa uongozi juu ya kutoa fedha za kutosha za usajili, huku nyota wa Real Madrid, Gareth Bale, akiendelea kuwa lengo lao la kwanza katika usajili mwezi huu.

Wakati huo huo, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, alikiri kuwa kwenye majaribio bila kuchoka ya kumshawishi Sanchez abaki Emirates, licha ya kwamba staa huyo amegoma kabisa kusaini mkataba mpya.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU