TORRES: COSTA ANAPASWA KUJIREKEBISHA

TORRES: COSTA ANAPASWA KUJIREKEBISHA

393
0
KUSHIRIKI
MADRID, Hispania

STRAIKA mkongwe wa klabu ya Atletico Madrid, Fernando Torres, amesema kuwa Diego Costa anatakiwa kutambua timu hiyo inamhitaji hivyo abadilike kitabia kuepuka kadi nyekundu zisizo na maana.

Tangu Costa arejee Atletico mwaka huu akitokea Chelsea, ameonesha ubora wake uwanjani lakini bado zile tabia zake hazijatoweka.

Wiki iliyopita straika huyo alioneshwa kadi ya pili ya njano kwa kosa la kushangilia bao jukwaani na mashabiki na tukio hilo limemwibua Torres ambaye alitoa neno lake kwa Costa, akimshauri kujifunza kutokana na makosa.

“Anatakiwa kujifunza ni vitu gani afanye na vingine vya kuachana navyo, sipendi kuona hilo likitokea tena kwa sababu tunamhitaji,” alisema.

“Tunamkubali sana Costa. Msimu ambao tulichukua Kombe la La Liga alicheza vizuri mno. Nina matumaini atafanya tena hivyo msimu huu, kufunga mabao na kutupa mataji,” aliongeza.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU