YERRY MINA AMFUATA COUTINHO BARCA

YERRY MINA AMFUATA COUTINHO BARCA

238
0
KUSHIRIKI
CATALAN, Hispania

KLABU ya Barcelona imekamilisha dili la kumsajili beki wa kati wa Palmeiras, Yerry Mina, kwa dau la uhamisho la pauni milioni 10.4.

Vinara hao wa La Liga walitangaza jana kuwa Mina alikubali kusaini mkataba wa miaka mitano na nusu na ripoti zilisema kuwa Mkolombia huyo anaenda kuziba pengo la Javier Mascherano ambaye anatarajiwa kujiunga na klabu ya Hebei China Fortune.

Mina anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa mwezi huu na Barcelona, baada ya Philippe Coutinho.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU