YANGA YAPEWA KIFAA CHA CAF

YANGA YAPEWA KIFAA CHA CAF

2297
0
KUSHIRIKI

NA SAADA SALIM

YANGA washindwe wenyewe kukiimarisha zaidi kikosi chao kitakachoshiriki michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwani wamefunguliwa milango na URA ya Uganda iwapo wanamtaka kiungo matata wa timu hiyo, Nicholas Kagaba.

Kagaba ni miongoni mwa wachezaji waliong’ara mno kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofikia tamati leo kwa mchezo wa fainali kati ya Azam na URA kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kiwango kilichoonyeshwa na Kagaba kwenye michuano hiyo, kiliwavutia viongozi wa Yanga na kumpigia hesabu kabla ya Kocha Mkuu wa URA, Ntaka Paul, kuruhusu Wanajangwani hao kumtwaa kiungo huyo mwenye kila aina ya sifa ya kuwachezea mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa kufahamu kuwa wana nafasi ya kuongeza wachezaji iwapo watavuka hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, vigogo wa Yanga wameona ni vema wakamalizana mapema na Kagaba wakiamini atawasaidia mno.

Habari kutoka kwa kigogo mmoja wa Yanga ameliambia BINGWA kuwa kuna mwenzao mmoja amebaki Zanzibar ili kumalizana na kiungo huyo.

Kigogo huyo alisema mchezaji huyo huenda…(Inaendelea kwenye gazeti)

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU