AZAM YATAMBA KUTWAA UBINGWA

AZAM YATAMBA KUTWAA UBINGWA

323
0
KUSHIRIKI

NA SAADA SALIM

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC, wametamba kuwachapa URA ya Uganda kwenye mchezo wa fainali wa michuano hiyo    utakaopigwa leo kwenye Uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar.

Ushindi katika mtanange wa leo utakaochezwa saa 2:30 usiku, utawafanya Azam waweke rekodi ya kunyakua taji hilo mara ya nne zaidi ya timu nyingine.

Azam imeweza kutinga hatua hiyo ya fainali baada ya kuwachapa Singida United bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa juzi Jumatano.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2013/2014, wameonyesha kiwango cha juu kwenye michuano hiyo, ikifanikiwa kumaliza mechi za Kundi A wakikusanya pointi tisa wakishinda mechi tatu na kufungwa moja dhidi ya URA, wakiruhusu mabao matatu na kufunga 11.

Kiwango hicho kinamfanya kocha wa Azam, Aristica Cioaba, kuamini kwamba wanaweza kubeba taji hilo kwa kuwachapa URA pamoja na kupoteza dhidi yao kwenye mchezo wa makundi.

Kocha huyo wa Romania, Cioaba amesema kuwa wamejiandaa vizuri na kazi iliyobakia ni vijana wake kumaliza kazi.

“Tumefika hapa kutokana na maandalizi mazuri ya timu yetu nzima na kujituma. Tunajua mechi ya fainali ni ngumu sana kwa kuwa URA watakuja na mipango tofauti, lakini…”

Kwa habari zaidi usikose nakala yako

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU