ENKA INATAKA KUMHARIBIA WILSHERE

ENKA INATAKA KUMHARIBIA WILSHERE

197
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

KWA mara nyingine tena kiungo Jack Wilshere anatarajiwa kukaa nje kutokana na jeraha la enka lililompata wakati akiitumikia klabu yake ya Arsenal dhidi ya Chelsea, katika mchezo wa nusu fainali ya Carabao Cup.

Ripoti zinasema kuwa kuna shaka kama Wilshere ataweza kucheza mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Bournemouth kesho.

Katika mchezo huo dhidi ya Chelsea uliomalizika kwa suluhu, Wilshere mwenye umri wa miaka 26 kwa sasa, alikabidhiwa kitambaa cha unahodha lakini baadaye wakati mchezo ukiendelea alikaa chini na kushika enka ya mguu wake wa kulia, na mawazo ya nuksi ya majeraha ikamrudia tena.

Wilshere ambaye alirejea mapema Agosti mwaka jana baada ya kupona jeraha jingine la mguu lililomkumba wakati akiitumikia Bournemouth kwa mkopo, alijitahidi kuendelea na mchezo huo baada ya kutibiwa nje lakini maumivu yalimlazimisha kutoka nje dakika 30 baadaye.

“Enka yake imepata mushkeli, sijajua atakaa nje kwa muda gani ila enka yake ndiyo imepata tatizo,” alisema kocha wake, Arsene Wenger, baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

“Kwa sasa tuna majeruhi watano na nina matumaini baadhi yao watarudi mapema. Nadhani atakayewahi ni Aaron Ramsey na itasaidia sana, kwani hatuna machaguo ya kutosha kwenye safu ya kiungo.

“Kama Wilshere asingeumia  tusingehangaika hivi.”

Hali ya Wilshere bado inaendelea kuchunguzwa na timu ya madaktari wa Arsenal, lakini kuna mashaka makubwa kama atacheza kesho.

Msimu huu Wenger aliona ni vyema kumtumia Wilshere kwenye mechi za Ligi ya Europa tu baada ya kupona, lakini baadaye hakuona tabu kumjumuisha kwenye kikosi cha Ligi Kuu kuanzia Oktoba mwaka jana ambapo hadi sasa ameshacheza mechi saba za ligi.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU