MAPYA YAIBULIWA KUDENGUA KWA OKWI

MAPYA YAIBULIWA KUDENGUA KWA OKWI

2779
0
KUSHIRIKI

NA MAREGESI NYAMAKA

MAPYA yameibuka juu ya tabia ya Emmanuel Okwi kuidengulia Simba ambapo hadi sasa hajarejea nchini akiwa kwao Uganda, kitendo kinachowakera mno wapenzi wa timu yake hiyo wakiwamo viongozi.

Okwi aliondoka nchini Novemba mwaka jana mara baada ya kusimamishwa kwa Ligi Kuu Tanzania Bara kupisha michuano ya Chalenji iliyofanyika Kenya, ambapo hadi sasa hajarejea kuungana na wenzake.

Juu ya kukosekana kwake katika kikosi cha Simba, ilielezwa kuwa Mganda huyo alikuwa akiuguza tatizo lililokuwa likimkabili la kifundo cha mguu, huku wengine wakidai ni amegoma kutokana na     kudai fedha za usajili kwani hakupewa zote wakati anasaini mkataba wa kuitumikia timu yake hiyo.

Mara kadhaa viongozi wa Simba wamekuwa wakipatwa na kigugumizi kila wanapoulizwa suala la Okwi, huku wengi wao wakionekana kutokuwa na habari zozote juu ya utoro wa nyota wao huyo.

Mbaya zaidi, Okwi amekuwa nje ya kikosi cha Simba wakati timu yake hiyo ikiwa inakabiliwa na mechi muhimu za Ligi Kuu Bara na hata michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofikia tamati leo visiwani Zanzibar kwa mechi ya fainali kati ya Azam na URA ya Uganda.

Lakini wakati mashabiki na viongozi wa Simba wakionekana kuwa katika sintofahamu juu ya Okwi, viongozi wa tawi la Simba la Kibondemaji lililopo Mbagala, Dar es Salaam linalojiita ‘Watu wa Mpira’, wameibuka na jipya juu ya sababu za kudengua kwa Mganda huyo.

Akizungumza na BINGWA juzi tawini kwao, Katibu Mkuu wa Watu wa Mpira hao, Banza Badatu, alisema kuwa … ndio chanzo cha nyodo za Okwi ndani ya kikosi chao hicho.

“Okwi ni mchezaji mzuri, wote tunampenda sana, lakini kutokana na hizi tabia zake, mara kaondoka, mara hivi, anatuumiza sana kwa kweli. (Inaendelea gazetini)

Kwa habari zaidi usikose nakala yako

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU