PRISONS KUWAKOSA WAWILI MBEYA DERBY

PRISONS KUWAKOSA WAWILI MBEYA DERBY

249
0
KUSHIRIKI

NA MARTIN MAZUGWA

TIMU ya Tanzania Prisons inatarajia kuwakosa nyota wawili wa kikosi cha kwanza, Lambert Sabiyanka na Kassim Khamis, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City unaojulikana kama Mbeya Derby, unaotarajia kupigwa kesho katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini humo.

Prisons wanatarajia kuwakosa viungo wao tegemeo kwa sababu mbalimbali, Sabiyanka anayetumikia adhabu ya kuwa nje kwa michezo mitatu kutokakana na kosa la kumpiga kiwiko mlinzi wa kulia wa Yanga, Juma Abdul, huku Khamis akisumbuliwa na majeraha ya goti aliyoyapata katika mashindano ya Challenge nchini Kenya.

Akizungumza na BINGWA jana, Katibu mkuu wa timu hiyo, Avintishi Abdallah, alisema kuwa wachezaji hao ni muhimu katika kikosi chao kutokana na mchango wao msimu huu, hivyo kukosekana katika mchezo mgumu kama huo ni pengo kubwa kwao.

“Unajua tuna mchezo mgumu mbele dhidi ya majirani zetu, hivyo kuwakosa wachezaji muhimu katika kikosi cha kwanza ni pengo ambalo si rahisi kuzibika,” alisema.

Alisema kuwa licha ya ugumu wa mchezo huo, kikosi chake kinaendelea vizuri na mazoezi katika kambi yao iliyopo Luanda, jijini Mbeya.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU