UMEMSIKIA MOBETTO KUHUSU PENZI LAKE?

UMEMSIKIA MOBETTO KUHUSU PENZI LAKE?

1222
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MREMBO anayefanya vizuri kwenye sekta ya  mitindo nchini, Hamissa Mobetto, amevunja ukimya na kuweka wazi hisia za kulikumbuka penzi la mwanamume aliyewahi kumpenda.

Mobetto ambaye yupo jijini Johanesburg, Afrika Kusini, alitumia mtandao wa SnapChat kuandika ujumbe wenye maneno ya kulikumbuka penzi alilowahi kupewa na mwanamume anayempenda lakini hivi sasa hamtaki tena.

“Roho zetu zilipendana, viburi vyetu vikatuachanisha, wakati mwingine nakumiss lakini moyo wangu hauumii tena kama ilivyokuwa mwanzo, nilikupa dunia yangu lakini ukaanzisha vita, unacheza na mapenzi kama uliyavumbua, sijui nimwamini nani kwenye safari ya penzi langu maana majanga,” aliandika mrembo huyo ambaye ni mzazi mwenza wa msanii, Diamond Platnumz.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU