‘TUNGEMKABA OKWI TU, BOCCO ANGEFUNGA NANE’

‘TUNGEMKABA OKWI TU, BOCCO ANGEFUNGA NANE’

3562
0
KUSHIRIKI

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA wa Ruvu Shooting, Abdulmutik Haji, amewamwagia sifa mabeki wake  kwa kufanikiwa kuwakaba washambuliaji wote hatari wa Simba, licha ya kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru juzi.

Akizungumza na BINGWA jana, Haji alisema  safu yake ya ulinzi ingemkamia Emmanuel Okwi na kuwaacha wengine, John Bocco angeweza kuwafunga mabao nane peke yake.

Haji  alisema mabeki wake walionyesha nidhamu kuliko mchezo uliopita  waliofungwa mabao 7-0, uliochezwa Agosti 26, mwaka jana katika uwanja huo.

“Kuna makosa yamejitokeza lakini beki alifanya kazi kubwa kwa kuonyesha nidhamu ya mchezo, zile kadi ni makosa mengine lakini nitakwenda kuyarekebisha kabla ya kucheza na Kagera Sugar,” alisema Haji.

Ruvu Shooting inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 14 baada ya kucheza michezo 16.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU