SNOOP DOGG KUACHIA GOSPO MACHI 16

SNOOP DOGG KUACHIA GOSPO MACHI 16

2299
0
KUSHIRIKI

 

LOS ANGELES, Marekani

MWAKA jana, mkali Snoop Dogg alisema anataka kugeukia muziki wa gospo na tayari mipango iko sawa kuhakikisha anajitosa kumwimbia ‘Bwana’.

Kwa mujibu wa supastaa huyo, mashabiki wake wajiandae kupokea albamu yake ya kwanza ya muziki wa Injili ifikapo Machi 16.

Dogg alisema itakuwa na nyimbo 32 na miongoni mwa wasanii aliowashirikisha ni Tye Tribbet, Faith Evans na Clark Sisters.

Akizungumzia uamuzi wake wa kuimba muziki wa gospo, nyota huyo alisema: “Ni kitu ambacho kimekuwa moyoni mwangu.”

“Sikuwa nikiimba kwa kuwa nilikuwa nikifanya kazi za ‘kigengsta’ sana. Nahisi nimekuwa nikitamani kwa muda mrefu na sasa ni wakati wa kufanya,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU