BUSTA RHYMES: ALBAMU MPYA ITAKUWA BALAA

BUSTA RHYMES: ALBAMU MPYA ITAKUWA BALAA

2278
0
KUSHIRIKI

LOS ANGELES, Marekani

RAPA mkongwe, Busta Rhymes, ametamba albamu yake mpya itakuwa gumzo katika soko la muziki duniani.

Akihojiwa na mtandao wa Billboard, supastaa huyo alisema ameandaa mzigo ambao hajawahi kuwa nao tangu alipoanza muziki.

Katika kuwaweka tayari mashabiki wake, Februari 2, Busta aliachia ngoma yake ‘Get It’ aliyowashirikisha Missy Elliott na Kelly Rowland.

“Kitu pekee ninachoweza kusema ni kwamba utakuwa ni mzigo ambao sijawahi kuufanya,” alisema Busta.

Aidha, aliongeza kuwa kwa kuwa hajaachia albamu tangu mwaka 2009, ana hamu ya kuliteka upya soko la muziki.

“Nimekuwa nikiifanyia kazi kwa miaka tisa,” alisema staa huyo na kudai kuwa jina la albamu hiyo atalitaweka hadharani hivi karibuni.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU