MWANASHERIA WA MEEK MILL AMJIA JUU HAKIMU

MWANASHERIA WA MEEK MILL AMJIA JUU HAKIMU

2224
0
KUSHIRIKI

LOS ANGELES, Marekani

BADO rapa Meek Mill anatumikia adhabu yake ya kifungo cha gerezani, lakini mwanasheria wake ameibuka kudai mteja wake hakutendewa haki.

Baada ya kubainika kumfanyia vurugu mmoja kati ya wafanyakazi wa ndege, msanii huyo alihukumiwa kifungo cha miaka miwili lakini adhabu hiyo inaweza kufikia miaka minne.

Hata hivyo, mwanasheria wake Joe Tacopina, alisema hakimu wa kike, Genece Brinkley, alimpa adhabu kubwa Meek kwa kuwa alikuwa na bifu na mwimbaji huyo.

Bada ya kusikia hivyo, naye hakimu Brinkley amejibu mapigo akisema atamfikisha mbele ya sheria Tacopina kwa kuwa kauli yake hiyo imelenga kumchafua.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU