PAYET, SARR KUIKOSA FAINALI EUROPA

PAYET, SARR KUIKOSA FAINALI EUROPA

4745
0
KUSHIRIKI

MARSEILLE, Ufaransa


 

HABARI mbaya kwa mashabiki wa klabu ya Marseille ni kwamba, kikosi chao huenda kikacheza fainali ya Ligi ya Europa bila mastaa wake, Dimitri Payet na Buona Sarr.

Marseille watashuka dimbani Mei 16, mwaka huu, kumalizana na Atletico Madrid, mchezo utakaoamua bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka huu.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, ililazimishwa sare ya mabao 3-3 na Guingamp, hivyo kukijiweka hatarini kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kiungo na nahodha, Payet, pamoja na beki wao mahiri, Sarr, ni nyota tegemeo katika kikosi hicho cha kwanza cha Marseille ambacho kimebakiwa na nafasi moja pekee itakayowawezesha kutinga ligi ya mabingwa.

Nafasi hiyo ni kuhakikisha wananyakua taji la Ligi ya Europa lakini inaonekana tayari ni ngumu iwapo watawakosa wachezaji hao.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU