UJENZI UWANJA WA SIMBA BUNJU UMEANZA

UJENZI UWANJA WA SIMBA BUNJU UMEANZA

6945
0
KUSHIRIKI

NA MWANDISHI WETU


Mkuu wa Kitengo cha Habari cha timu ya soka ya Simba Sc, Haji Manara amesema mazungumzo na mkandarasi atakaye simamia ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo uliopo Bunju yamekamilika ndiyo maana ujenzi wake umeanza.
“Tumeanza ujenzi wa uwanja huo na tutawapeleka waandishi wa habari wakajionee mambo yanavyoendelea katika ujenzi,” alisema Manara.
Klabu ya Simba inategemea kuondoka Dar es Salaam hivi karibuni kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi Semptemba 15 dhidi ya timu ya Ndanda Fc na baada ya mechi hiyo itakwenda Kanda ya Ziwa kucheza na Mbao FC.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU